Simba Sports Club
News

Alichosema Robertinho baada ya ushindi wa jana dhidi ya Vipers

8 Mar 2023

Robertinho amesema haikuwa mechi rahisi kwakuwa Vipers walikuwa wanatupa presha mara kwa mara lakini wachezaji wetu walikuwa makini muda wote.

Robertinho ameongeza kuwa tumecheza kwa umoja kuanzia kwa walinzi, viungo hadi kwa washambuliaji na ndicho kimesababisha ushindi upatikane.

Advertisement

"Nawapongeza wachezaji wangu kwa jitihada walizofanya, tumecheza kwa umoja kuanzia nyuma hadi mbele hilo ndilo jambo zuri.

"Kwenye Ligi ya Mabingwa hakuna mechi rahisi hata sisi tulijipanga kwa hilo kutoka kwa Vipers, kinachotakiwa ni kupata pointi tatu," amesema Robertinho.

Back to homepage
Share this story