Simba Sports Club
News

Alichosema Pablo kuhusu mchezo dhidi ya Azam

17 May 2022

Pablo amesema tuna wachezaji wazuri katika kila idara kama ilivyo kwa Azam hivyo anatarajia mchezo mzuri kutokana na Uwanja wa Azam Complex ambao utatumika kuwa bora katika eneo la kuchezea.

Pablo ameongeza kuwa katika mechi zetu zilizopita tuliwakosa wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza kutokana na kuwa majeruhi lakini baadhi wamerejea na wapo tayari kwa mechi ya kesho.

Advertisement

"Kwetu sisi kila mchezo ni fainali tunahitaji kushinda ili kuendelea kupunguza tofauti ya alama zilizopo na vinara. Tunafahamu mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa Azam lakini tupo tayari kupambania pointi tatu.

"Tuliwafunga mchezo wa mzunguko wa kwanza na kwenye Kombe la Mapinduzi pia lakini haimaanishi itakuwa rahisi bali tutapambana," amesema Pablo.

Back to homepage
Share this story