Simba Sports Club
News

Alichosema Mgosi kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya JKT Queens

11 Dec 2023

Mgosi amesema JKT walitupokonya taji msimu uliopita kwa alama moja kwahiyo mchezo wa kesho utatoa picha kuelekea 2023/24.

Mgosi ameongeza kuwa kikosi cha Queens kipo tayari na tumefanikiwa kuwaona JKT walivyocheza mchezo uliopigwa dhidi ya Fountain Gate ambapo tumebaini ubora na mapungufu yao.

"Itakuwa mechi ngumu, JKT Queens ni mabingwa wa ligi msimu uliopita walituvua taji kwa tofauti ya alama moja nasi tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kuchukua ubingwa," amesema Mgosi.

Advertisement

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji, mlinzi wa kati Vivian Corazone amesema wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo huku akikiri haitakuwa mechi rahisi.

"Sisi kama wachezaji tumejiandaa kwa ajili mchezo huo, haitakuwa mechi rahisi lakini tupo tayari na lengo letu ni kuchukua taji," amesema Corazone.

Back to homepage
Share this story