Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema baada ya timu kufika nchini Morocco kikosi kitakuwa na muda wa siku tatu za maandalizi kabla ya mchezo wetu dhidi ya RS Berkane utakaopigiwa Jumapili.
Matola amesema baada ya kufika jijini Casablanca kikosi kitafanya mazoezi ya utimamu wa mwili (recovery) kwa sababu tangu tumalize mchezo dhidi ya US Gendarmerie Nationale hakijapata muda wa kupumzika vizuri.
Advertisement
Matola amesema kikosi kitaweka kambi ya muda hapa Casablanca kabla ya kwenda mji wa Berkane ambapo mchezo wetu utapigwa.
"Tunamshukuru Mungu tumefika salama Morocco kikosi kitafanya mazoezi ya utimamu wa mwili kwa sababu kwa siku mbili hatujafanya mazoezi, tuna siku tatu tu za kujiandaa kabla ya mchezo," amesema Matola.