LTyron ambaye ni mwenyeji wa Afrika Kusini amekiri mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani hasa wakiwa nyumbani lakini tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri.
Tyron ameongeza kuwa kama tuliweza kuwafunga katika mchezo wa kwanza nyumbani basi pia tunaweza kukaza ugenini na tutafanikiwa kuingia nusu fainali.
"Tumewaandaa wachezaji kimwili na kiakili kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Orlando. Tunajua tupo ugenini na wenyeji wetu ni timu bora lakini hakuna kinachoshindikana kwenye mpira.
"Sisi kama benchi la ufundi tumewapa morali wachezaji na kuwaambia kuacha kufikiria mechi zetu za nyuma za ugenini ambazo tumekuwa hatufanyi vizuri badala yake waweke mkazo kwenye mechi ya kesho. Tunaamini tunaweza kupata matokeo mazuri," amesema Tyron.