Simba Sports Club
News

Alichosema Kocha Mgunda kuelekea mchezo wa kesho

13 Sep 2022

Mgunda amesema baada ya kurudi kutoka Malawi timu imefanya mazoezi siku mbili jana na leo kabla ya kuanza safari kuelekea Mbeya.

Mgunda amewataja wachezaji wawili viungo wakabaji Victor Akpan na Sadio Kanoute kuwa hawatakuwa sehemu ya mchezo kwa sababu tofauti.

Advertisement

Akpan anaendelea kuuguza majeraha wakati Kanoute anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano hivyo kanuni haziruhusu kuwa sehemu ya mchezo wa kesho.

"Kikosi kipo kwenye hali nzuri, tumepata siku mbili za kufanya mazoezi jana na leo, tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tupo tayari kupambana kuhakikisha tunarudi na pointi zote tatu," amesema Mgunda.

Back to homepage
Share this story