Mgunda ameyasema hayo muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuelekea mkoani Kagera kuelekea mchezo huo ambao utapigwa kesho saa 10 jioni katika Uwanja wa Kaitaba.
Mgunda amesema utakuwa mchezo mgumu na tunawaheshimu Kagera kutokana na ubora walionao lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi.
Mgunda amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo wa kesho na tutaingia uwanjani kwa lengo la kutafuta pointi tatu licha ya ugumu walionao Kagera.
"Maandalizi yamekamilika, tunaondoka tukiwa tunajua tunaenda kukutana na timu ngumu. Tahadhari zote za kupambana na timu bora zimechukuliwa."
"Kila timu inayoshiriki Ligi ni bora, na sisi Simba tumejipanga kukabiliana na yoyote na tunawapa heshima sawa huku malengo yetu yakiwa kupata matokeo chanya," amesema Mgunda.