Simba Sports Club
News

Alichosema Kocha Mgosi baada ya ushindi dhidi ya Alliance

27 Jan 2024

Mgosi amesema faida ya kupata ushindi mnono ni kuongeza hamasa katika mechi inayofuata hasa ukizingatia mchezo uliopita tulitoka sare.

Mgosi ameongeza kuwa ligi ya msimu huu ni ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda kila mchezo ingawa haitakuwa kazi rahisi.

Advertisement

"Ligi ni ngumu na kila timu imejiandaa vizuri, tunahitaji kushinda kila mchezo na kucheza soka safi pia ili kuweza kurejesha ubingwa wetu."

"Ushindi dhidi ya Alliance utaongeza hamasa kuelekea mechi yetu ijayo, timu inaposhinda kwa mabao mengi kama Leo unaongeza hamasa kwa wachezaji," amesema Magosi.

Back to homepage
Share this story