Matola amesema Ligi ya msimu huu itakuwa ngumu kutokana na kila timu kujipanga vizuri na tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Fountain Gate lakini tupo tayari kupambana kwa ajili ya alama tatu.
Matola ameongeza kuwa malengo yetu msimu huu ni kuhakikisha tunatwaa ubingwa wa Ligi kwahiyo tunapaswa kuanza vizuri kwa kupata alama tatu mbele ya Fountain Gate ingawa haitakuwa kazi rahisi.
"Maandalizi yetu yamekwenda vizuri na tupo tayari kuhakikisha tunapata alama tatu katika mchezo wa kesho dhidi ya Fountain Gate," amesema Seleman.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kulia, David Kameta 'Duchu' amesema wapo tayari kufuata malekezo watakayopewa na walimu ili kuweza kufikia malengo ya kupata alama zote tatu nyumbani.
"Kila mchezaji anatambua kuwa hautakuwa mchezo rahisi lakini tupo tayari kuhakikisha tunafuata maelekezo tutakayopewa na walimu ili kuweza kupata alama tatu," amesema Duchu.