Simba Sports Club
News Videos

Alichosema kocha Matola kuelekea mchezo dhidi ya Coastal

1 Apr 2026

Matola amesema mchezo huo utakuwa mgumu kwasababu ya uimara wa Coastal ambao unatokana na aina ya wachezaji mchanganyiko vijana na wenye uzoefu huku wengine wakiwa wamewahi kucheza kwetu.

Matola ameongeza kuwa mchezo dhidi ya Coastal haujawahi kuwa mwepesi kwetu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapata alama tatu muhimu kwenye mtanange huo.

Kuhusu hali za wachezaji Matola amesema ukiacha Yakoub Suleiman, Abdulazak Hamza na Wilson Nangu ambao watakuwa nje hadi mwisho wa msimu hakuna ambaye atakosekana kwenye mchezo wa kesho.

Advertisement

"Utakuwa mchezo mgumu, tunawaheshimu Coastal na mara zote wamekuwa wakitupa upinzani mkubwa lakini tumejipanga kuhakikisha tunawakabili na kupata alama tatu," amesema Matola.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mkabaji, Daud Semfuko amesema pamoja na ugumu ambao tunategemea kukutana nao kutoka kwa Coastal lakini tumejipanga kikamilifu kupata ushindi nyumbani.

"Kwa upande wetu kama wachezaji kila mmoja yupo tayari kuhakikisha anapambana mpaka mwisho kuisaidia timu kupata ushindi kwenye mchezo wa kesho, tunafahamu haitakuwa rahisi lakini tupo tayari," amesema Semfuko.

Back to homepage
Share this story