Cadena amesema hali ya wachezaji ipo vizuri na wameshiriki vema mazoezi ya maandalizi ambapo anaamini wataweza kutupa ushindi kwenye mchezo wa kesho.
Cadena ameongeza kuwa timu inapopoteza mchezo hakuna mtu anakuwa furaha lakini baada ya kubadili benchi la ufundi hali imetulia na kila mmoja ameweka nguvu katika mchezo wa kesho.
Advertisement
"Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, hali za wachezaji zipo vizuri morali ipo juu, naamini kikosi chetu kitatupa matokeo chanya kesho," amesema Cadena.
Akizungumzia hali za wachezaji Cadena amesema "mlinda mlango Aishi Manula alipata maumivu ya mguu akiwa na Taifa Stars na Clatous Chama amerejea kutoka Zambia usiku wa kumkia leo hivyo tutaangailia kwenye mazoezi ya mwisho leo jioni kama tutawatumia kesho."