Simba Sports Club
News

Alichosema Kocha Basigi kuelekea mchezo dhidi ya Bunda Queens

26 Dec 2024

Basigi amesema hategemei kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi kwakuwa mara zote timu ya ushindi huwa haibadiliki.

Busigi amesema anategemea kutumia kikosi kilichotupa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mashujaa Queens wiki iliyopita kama kitakuwa na mabadiliko basi ni wachezaji wawili au watatu.

Advertisement

"Tupo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Bunda, furaha yetu ni kwamba tumewahi kufika huku na tumepata nafasi ya kuzoea mazingira," amesema Kocha Basigi.

Kikosi cha Queens kimefanya mazoezi ya mwisho jioni katika Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara tayari kwa mchezo wa kesho.

Back to homepage
Share this story