Simba Sports Club
News

Alichosema Kocha Basigi kuelekea Derby Kesho

12 Nov 2024

Kocha Basigi amesema anaamini utakuwa mchezo mzuri na mgumu kutokana na wapinzani wanaokutana lakini Queens imepata maandalizi mazuri.

Kocha Basigi ameongeza kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo huku malengo yakiwa kupata ushindi.

"Utakuwa mchezo mgumu, tunajua tutakutana na timu bora na hii ni 'derby' na haijawahi kuwa nyepesi lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapata pointi zote tatu," amesema Kocha Basigi.

Advertisement

Akiongea kwa niaba ya wachezaji kiungo mkongwe, Amina Bilal amesema wapo tayari kufuata maelekezo watayopewa na walimu ili kuwapa furaha Wanasimba.

"Sisi tupo tayari kwa mchezo wa kesho, tunajua itakuwa mechi ngumu Yanga ni timu imara, lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda," amesema Amina.

Tutaingia katika mchezo wa kesho tukiwa na kumbukumbu nzuri ya kuwa kileleni mwa msimamo baada ya kushinda mechi zote tatu za mwanzo.

Back to homepage
Share this story