Barker amesema kwa jinsi alivyoutazama mchezo wa jana dhidi ya Muembe Makumbi anaamini hata kesho upinzani utakuwa mkubwa.
Kocha Barker ameenda mbali zaidi kwa kusema malengo yetu kwenye michuano hii ni kuhakikisha tunatwaa taji ingawa tunategemea kupata upinzani mkubwa.
"Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, kikosi kipo kwenye hali nzuri. Tunafahamu michuano hii migumu lakini tunahitaji kutwaa ubingwa," amesema kocha Barker.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mshambuliaji, Awesu Awesu amesema wapo tayari kupambania mpaka mwisho ili kupata ushindi kwenye mchezo wa kesho.
"Kila timu inayokutana na Simba lazima ijipange vizuri lakini sisi kama wachezaji tunalijua hilo na tupo tayari kufuata maelekezo tutakayopewa na benchi la ufundi ili kupata ushindi," amesema Awesu.