Simba Sports Club
News

Alichosema Kapombe baada ya kuwasili Algeria

4 Dec 2024

Kapombe amesema siku mbili za mazoezi ambazo watazipata watazitumia vizuri kuhakikisha tunapata matokeo chanya ugenini.

Akizungumza kuhusu hali ya hewa ya Algeria, Kapombe amesema ni baridi kali lakini siku zilizobaki kabla ya mchezo zitasaidia kuwafanya kuzoea mazingira.

Advertisement

"Hali ya hewa ni baridi kali lakini tuna siku mbili za kufanya mazoezi pamoja na kuzoea mazingira tunaamini hadi kufika siku ya mchezo tutakuwa tumeshazoea," amesema Kapombe.

Kikosi chetu kimewasili salama hapa Algeria usiku huu na kesho kitaanza programu ya mazoezi.

Back to homepage
Share this story