Elizabeth amesema wachezaji wote wanafahamu utakuwa mchezo mgumu na tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Fountain Gate lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.
Elizabeth ameongeza kuwa pamoja na ugumu ambao tutakutana bao lakini Simba Queens ina uzoefu mkubwa na tutautumia ili kupata matokeo chanya.
Advertisement
"Tupo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Fountain Gate sisi kama wachezaji malengo yetu ni kuhakikisha tunapata ushindi," amesema Elizabeth.
Kuhusu hali ya hewa ya Manyara, Elizabeth amesema kuna baridi tofauti na Dar es Salaam lakini haitakuwa changamoto kubwa kwakuwa tumeshawahi kukutana nayo mara zote.