Simba Sports Club
News

Alichosema Benchikha baada ya ushindi dhidi ya Kagera

15 Dec 2023

Benchikha amesema uwanja haukuwa rafiki na kutunyima kucheza soka safi lakini hata hivyo amefurahi kwa ushindi huo mnono.

Aidha Benchikha amesema Kagera ni timu nzuri na walitupa ushindani mkubwa lakini tulikuwa bora na kufanikiwa kuibuka na ushindi huo.

Advertisement

"Tumecheza vizuri, nawapongeza wachezaji wangu. Tulimiliki sehemu kubwa ya mchezo lakini uwanja haukuwa rafiki na kutunyima kucheza soka safi

"Kagera ni timu nzuri wanacheza soka safi na walitupa ushindani mkubwa ingawa sisi tulikuwa bora ndio maana tumepata ushindi," amesema Benchikha.

Back to homepage
Share this story