Barker amesema tuna wajibu wa kucheza soka safi na kupata matokeo ambayo Simba pamoja na mashabiki wetu tunastahili.
Barker ameongeza kuwa mchezo wa kesho utakuwa mgumu kutokana na mpizani ambaye tunakutana nae huku akiwa yupo nyumbani lakini hata hivyo tupo tayari kupambana.
"Utakuwa mchezo mgumu, tunaenda kukutana na mpizani mgumu lakini tunapaswa kupambana ili kupata matokeo ambayo mashabiki wa Simba wanataraji kuyapata," amesema kocha Barker.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mshambuliaji, Neo Maema amesema matokeo pekee ambayo tunayahitaji ni kupata alama tatu katika mchezo wa kesho ingawa haitakuwa kazi rahisi.
"Wachezaji wote tupo tayari kwa mchezo wa kesho, tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tunahitaji matokeo ya alama tatu pekee," amesema Maema.