Mnuka amekuwa kwenye kiwango bora msimu uliopita na ndiye kinara wa mabao baada ya kupachika wavuni mabao 20.
Mchango wa Mnuka katika Ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake msimu uliopita ni mkubwa maana ukiachana na mabao aliyofunga pia amehusika katika kupatikana kwa mengine.