Banda (23) alisajiliwa Agosti 3, mwaka 2021 kutoka Nyasa Big Bullets ya nchini Malawi kwa mkataba wa miaka mitatu.
Katika kipindi cha miaka miwili tulichokuwa na Banda amekuwa mchezaji muhimu ambaye alikuwa akiongeza kasi katika safu ya ushambuliaji.
Advertisement
Uongozi wa klabu unathamini mchango wa Banda kwenye timu katika kipindi chote alichodumu nasi.
Simba inamshukuru na kumtakia heri Banda katika maisha yake mapya ya soka nje ya Simba.