Ahmed amesema mashabiki wetu wamejitokeza kwa wingi na hilo ndilo huwa wanafanya kila mara na tunajivunia sana kuwa nao.
Ahmed ameongeza kuwa sio Tanzania tu iliyoshtuka bali ni Afrika nzima ndio maana Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limechagua sisi tufanye uzinduzi wa michuano hii sababu wanajua tunaweza kuitendea haki.
"Zoezi letu la ufunguzi wa hamasa kuelekea michuano ya African Football League limekamilika na limefana kama tulivyotarajia.
"Wanasimba wamekuja kwa wingi na wamefurahi kwa kila kilichotokea. Shughuli ndio imeanza tutahakikisha kila Mtanzania anafahamu kuwa Simba anacheza na Al Ahly kwenye ufunguzi wa AFL," amesema Ahmed.
Ahmed ameongeza kuwa "wiki inayoanza Jumatatu tutakuwa na mishemishe mingi za hamasa mpaka Ijumaa tutakapokutana na Al Ahly."