Ahmed amesema sababu ya kufungiwa kucheza bila mashabiki ni mchezo ni dhidi ya Al Masry mashabiki wetu walifanya fujo uwanjani na kuna mashabiki waliwasha moto ambapo adhabu hiyo inakwenda pamoja na faini ya Dola 50,000 takribani Shilingi milioni 120.
Ahmed ameongeza kuwa maandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri na kikosi kimeingia kambini jana baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Fountain Gate FC ambao tuliibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Ahmed ameweka wazi kuwa mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka Niger huku wapinzani Gaborone wakiwa tayari wamewasili nchini.
"Nipo hapa kuwathibitishia kwamba mechi yetu ya Jumapili haitakuwa na mashabiki kutumikia adhabu ya CAF kutokana na fujo zilizotokea kwenye mchezo dhidi ya Al Masri.
"Tayari wageni wetu Gaborone United wamewasili nchiji alfajiri ya leo, mambo yote yamekwenda vizuri na watafanya mazoezi leo na kesho," amesema Ahmed.
Kuhusu waamuzi Ahmed amesema "mchezo wetu wa Jumapili utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Niger wapo njiani na wataingia nchini muda wowote kutoka sasa."