Ahmed ameyasema hayo katika Uzinduzi wa hamasa kuelekea mchezo huo wa Robo Fainali zilizofanyika katika Tawi la Wekundu wa Chalinze.
Ahmed amesema Wydad ni timu kubwa na wana historia nzuri Afrika lakini kama tutaungana na kujitokeza kwa wingi uwanjani Jumamosi hakuna namna Waarabu hao watatoka Jumamosi kwa Mkapa.
"Tunaka kuandika histori nyingine ya kumvua mtu ubingwa kama tulivyofanya mwaka 2003 ndio maana kila Mwanasimba anatakiwa kuwa sehemu hili. Wydad ni timu kubwa lakini tukiungana hata wakija Wamorocco wote kwa Mkapa hawatoki."
"Kwa sasa kufika robo fainali sio mafanikio kwetu tunahitaji kuvuka kwenda nusu fainali hilo linawezekana kama kila Mwanasimba atatimiza majukumu yake Jumamosi," amesema Ahmed.
Ahmed amewashukuru Wanasimba wote waliojitokeza kwa wingi katika Uzinduzi huo pamoja na wenyeji wetu wa Wekundu wa Chalinze kwa maandalizi na ukaribisho mzuri.
"Kwa niaba ya mashabiki wote tuliopo hapa nawashukuru Wekundu wa Chalinze kwa mapokezi makubwa, mmetuheshimisha na nawaomba mjitokeze kwa wingi uwanjani Jumamosi," amesema Ahmed.