Simba Sports Club
News

Ahmed: Tumeweka Viingilio rafiki, Wanasimba tukutane kwa Mkapa

10 Dec 2024

Mchezo dhidi ya CS Sfaxien ambao utakuwa ni watatu wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika utapigwa Jumapili ya Disemba 15, saa 10 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ahmed amesema kiingilio cha chini kitakuwa Shilingi 3000 ambacho kila Mwanasimba ana uwezo wa kumudu kulipa na malengo yetu ni kuhakikisha Uwanja unajaa.

Ahmed amesema tukijitokeza kwa wingi na kuujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa hakuna namna yoyote CS Sfaxien watachomoka.

"Tupo hapa kwa ajili ya dhumuni moja ya kuhakikisha tunaujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili. Wanasimba kwa umoja wetu tukijitokeza kwa wingi uwanjani kuwapa sapoti wachezaji tuna uhakika wa kupata pointi tatu nyumbani," amesema Ahmed.

Hivi hapa Viingilio kamili vilivyotangazwa:

Advertisement

Mzunguko Sh. 3000

Machungwa Sh. 5000

VIP C Sh. 10,000

VIP B Sh. 20,000

VIP A Sh. 30,000

Back to homepage
Share this story