Ahmed ameyasema hayo muda mfupi baada kula chakula cha mchana na watoto yatima wa kutoka Kituo cha Hiari kilichopo Mbagala ikiwa ni sehemu ya hamasa kuelekea mchezo wa Jumapili.
Ahmed ameongeza mchezo wa Jumapili sio wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohamed Dewji 'Mo' wala Murtaza Mangungu bali ni ya kila Mwanasimba kuhakikisha anafika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
"Kwa upande wa Menejimeti, benchi la ufundi na wachezaji tumemaliza majukumu yetu kilochabaki na kila Mwanasimba kujitokeza katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili kuhakikisha tunawakaanga vilivyo Al Ahli Tripoli," amesema Ahmed.
Akizungumzia hali ya kikosi Ahmed amesema "wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo wa Jumapili isipokuwa mlinda mlango Ayoub Lakred ambaye anaendelea kupona majeraha."