Simba Sports Club
News

Ahmed: Mwanasimba yoyote asibaki nyumbani siku ya Jumapili

11 Dec 2024

Ahmed ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa hamasa kuelekea mchezo huo uliofanyika katika Tawi la Kapu la Magoli, Tandika Dar es Salaam.

Ahmed amesema kila Mwanasimba ana jukumu la kuhakikisha anaisaidia timu kutinga robo fainali na hilo litawezekana kama tukishinda katika mechi zetu za nyumbani.

Ahmed ameongeza kuwa Uongozi kwa kuthamini mchango wa mashabiki kwenye mchezo dhidi ya CS Sfaxien umeweka kiingilio cha chini Shilingi 3000 ili kila Mwanasimba aweze kumudu kukata tiketi na kuingia uwanjani.

Advertisement

"Tupo hapa kwa lengo moja la kuhamasisha mashabiki wajitojeze kwa wingi uwanjani kuwapa sapoti wachezaji ili kupata ushindi."

"Kwenye michuano hii kila timu inatakiwa kushinda mechi zake za nyumbani ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali na wachezaji peke yao hawawezi bila sapoti ya mashabiki," amesema Ahmed.

Back to homepage
Share this story