Ahmed ameyasema wakati akiongea na Wanasimba wa Tawi la Kwa Kisasi lililopo Mwanyanya, Zanzibar ambapo amebainisha kuwa malengo hayo yatakamilika kama tutakuwa wamoja na kuhakikisha tunavuka na kuingia fainali kwa kuitoa Stellenbosch.
Ahmed ameenda mbali zaidi kwa kusema mwasisi wa jina la Simba ni Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kwahiyo itakuwa jambo jema kama safari ya kuelekea kutwaa ubingwa huo kuanzia Zanzibar.
“Mwaka huu hatuhitaji kingine chochote zaidi ya Simba kwenda fainali ya Kombe la Shirikisho. Kwa ufupi tunataka ubingwa wa kombe la Shirikisho na hilo linawezekana.”
“Hata jina la Simba liliasisiwa na Hayati Abeid Amani Karume hivyo Simba ilianzishwa na Wazanzibari, maana yake Simba na Zanzibar ni damdam, na hii haiwezi kuwa kazi ngumu kwa Wazanzibari kuipeleka Simba fainali," amesema Ahmed.
Ahmed ameongeza kuwa "Fainali inapatikana kwa michezo miwili lakini sisi tunataka kuimaliza hapa hapa Zanzibar, tunataka kupata ushindi mkubwa ili Mnyama awe kwenye nafasi ya kwenda fainali."