Simba Sports Club
News

Ahmed: Msimu huu utakuwa bora kwetu

30 Aug 2025

Ahmed ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Simba uliofaanyika katika uwanja wa Wambi, Mafinga mkoani Iringa.

Ahmed ameongeza kuwa ndani ya kikosi chetu kwenye kila nafasi kuna zaidi ya wachezaji wawili bora huku safu ya ushambuliaji balaa zaidi.

“Katikati yupo Yusuph Kagoma lakini tumemuongezea mtu anaitwa Kunta Kinte, Ila eneo la mbele ndio kuna balaa zaidi, kuanzia namba nane kwenda mbele kumejitosheleza.

Advertisement

"Kama una shamba la mbao mwaka huu unaweza kubet. Kuanzia kwa Jean Charles Ahoua, Neo Maema, Elie Mpanzu, sijamtaja Jonathan Sowah wala mfalme Gomez (Seleman Mwalimu), itoshe kusema mwaka huu timu tunayo.

Ahmed ameongeza kuwa "Majonzi tuliyopitia kwa miaka minne huu ndio mwisho wake, Wanasimba tembeeni vifua mbele wakati wa furaha umewadia.”

Back to homepage
Share this story