Ahmed ametangaza hilo katika Uzinduzi wa hamasa wa Tawi la Wekundu wa Migombani Kiwalani Dar es Salaam.
Ahmed amesema mara zote amekuwa akiwatangaza wachezaji na watu mbalimbali kwenye mechi zetu za Kimataifa na safari hii zamu yake.
Advertisement
"Mgeni Rasmi katika mchezo wetu Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravo utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumatano saa 10 jioni ni mimi mwenyewe Ahmed Ally."
"Ni mchezo muhimu kwetu, tunahitaji kupata pointi tatu hasa ukizingatia tupo nyumbani ndio tupo hapa kuwahamasisha kwa ajili ya kuja uwanjani kuipa sapoti timu. Tunawaamini wachezaji wetu wapo tayari kutupa furaha," amesema Ahmed.