Simba Sports Club
News

Ahmed: Mashabiki njooni kwa wingi kwa Mkapa Jumapili

16 Sep 2022

Ahmed amesema Simba tuna rekodi ya kujaza uwanja hasa tunaposhiriki michuano hii hatu inayosababisha kuogopwa na kila timu inayokanyaga ardhi ya Tanzania.

Ahmed ameongeza kuwa mashabiki wanaweza kujaza uwanja lakini wanashangilia kwa vipindi ambapo amewaomba kushangilia kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo.

"Jumapili tuna jambo letu kwa Mkapa, Wanasimba wenzangu nawaomba mje kwa wingi ili Nyasa Big Bullets wakiwa wanaingia tu uwanjani wajue kabisa wanaenda kuvuta pumzi ya moto.

Advertisement

"Kasumba moja waliyonayo mashabiki wetu ni kushangilia kwa wakati mpaka bao au mtu kupigwa chenga, hii tunatakiwa kuibadilisha, tunataka kutengeneza utaratibu wa mashabiki kuhanikiza mwanzo mwisho ili tuingie anga la klabu kubwa duniani.

"Juzi kwenye mchezo wetu dhidi Prisons kule Sokoine Mbeya kuna muda uwanja ulikuwa kimya kabisa kiasi kwamba mtu akipita nje anaweza asijue ndani kinaendelea nini, kwa hiyo tunapaswa kubadilika ili kuwachanganya wapinzani," amesema Ahmed.

Back to homepage
Share this story