Simba Sports Club
News

Ahmed: Jumanne iwe mvua iwe jua ushindi lazima kwa Mkapa

5 Mar 2023

Ahmed amesema ushindi dhidi ya Vipers utatuongezea nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali kwakuwa tutakuwa tumefikisha pointi sita.

Ahmed amesisitiza kuwa ushindi dhidi ya Vipers ni jukumu la Wanasimba wote kuanzia viongozi, benchi la fundi, wachezaji mpaka mashabiki na kila mmoja anapaswa kutimiza nafasi yake.

Advertisement

"Jumanne tuna jukumu zito Wanasimba, tunahitaji kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu. Ni matumaini yetu kila mmoja akitimiza jukumu lake Vipers hatoboi.

"Siku ya mchezo tumeteua jukwaa la chini ya TV kubwa pale kwa Mkapa, vikundi vyote vya hamasa vitakaa pale au yoyote anayejiweza hatuta pumzika dakika zote 90," amesema Ahmed.

Back to homepage
Share this story