Ahmed amesema Wekundu wa Kibamba wameibeba shughuli na wamejitokeza na hamasa zimefana.
Zoezi la hamasa limeanza katika Tawi la Mpira Pesa Magomeni Mikumi saa nne asubuhi kabla ya kuelekea Mbezi Mpaka Kibamba.
“Tumezunguka katika matawi mengi tumeshuhudia hamasa nyingi lakini Wekundu wa Kibamba maandalizi yenu ya dunia nyingine," amesema Ahmed.
Advertisement
Ahmed ameendelea kusisitiza mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani na kwa umoja tulionao tunaamini tuna nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya nusu fainali.
"Al Ahly pamoja na ukubwa wake wote na uzoefu wake wote safari hii Mnyama anaenda Nusu Fainali. Hii ni mechi ya kufa na kupona afe yeye tupone sisi, kwa mapenzi yake Mungu tunaenda nusu fainali," amesema Ahmed.