Simba Sports Club
News

Ahmed awatoa hofu Wanasimba mbele ya Waangola Jumapili

20 Nov 2025

Ahmed amesema kujiamini huko kunatokana na ubora wa kikosi chetu pamoja na benchi la ufundi lakini mashabiki wana umuhimu mkubwa ili malengo hayo yaweze kufikiwa.

Ahmed ameyasema hayo Goba jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ya pili ya hamasa kuelekea mchezo huo muhimu ambao amekiri tunaenda kukutana na timu imara.

“Tunahitaji kuanza vizuri hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini hatuwezi kufanikiwa kama kila mmoja hatimizi majukumu yake kwa asilimia 100. Viongozi waatimiza jukumu lao na wewe shabiki wa kawaida timiza wajibu wako na wajibu wako ni kununua tiketi na kuja uwanjani.”

Advertisement

“Hatuna mashaka sisi tutashinda kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu lakini ili tushinde vizuri ni wewe njoo uwanjani. Kwanza unabaki nyumbani unafanya nini? Awe babu, awe bibi, awe kijana, awe mvulana hata wewe binti mdogo njoo Benjamin Mkapa," amesema Ahmed.

Ahmed ameongeza kuwa "Kama huna kiingilio mfate mwenzio aokoe jahazi na wewe mwenye kipato cha kutosha mfate mwenzio ambaye hana mje Mkapa kwa pamoja."

Back to homepage
Share this story