Ahmed amesema ubora wa kikosi tulionao tunaweza kupata matokeo ya ushindi kwenye uwanja wowote kwahihiyo Wanasimba hawapaswi kuwa wanyonge baada ya mechi kutopigwa Benjamin Mkapa.
"Kuna Wanasimba wameanza kuingia unyonge kutokana na mechi kutopigwa Benjamin Mkapa kwakuwa wanafahamu Kwa Mkapa hatoki mtu, lakini Simba hii ni bora na unaweza kushinda kwenye uwanja wowote," amesema Ahmed.
Ahmed ametoa ufafanuzi wa jinsi ya ununuzi wa tiketi kuelekea mchezo huo ambao utaanza saa 10 jioni katika Uwanja wa Amaan ambao unaingiza mashabiki zaidi ya 15,000.
“Kwa ndugu zangu wa Zanzibar ambao wamezoea kununua tiketi za karatasi kwasasa wanaweza kununua tiketi za N-Card na ukawa nayo hadi siku ya mchezo. Siku ya mchezo tiketi hazitauzwa nje ya uwanja na maeneo mengine yataendelea, utaratibu huu ni wa CAF. Yeyote ambaye anahitaji tiketi anunue tiketi sasa," amesema Ahmed.