Ahmed amesema baada ya kufanikiwa kuwa Tawi sasa jambo lililo mbele yao ni kuhakikisha wanalifanya kuwa hai kwa kushiriki matukio mbalimbali ya klabu kama kuhudhuria mechi uwanjani.
Ahmed ameongeza kuwa ili tawi hilo kuwa hai nakuzidi kuwa maarufu ni kuhakikisha wanashiriki masuala yote ya klabu ikiwemo kusafiri kwenda mikoani kwa ajili ya kwenda kuisapoti timu.
"Tayari mmeshakuwa Wanasimba kamili, sasa mnatakiwa kulifanya Tawi lenu linakuwa hai kwa kusafiri mikoani kama ilivyo Wekundu wa Terminal, Kamati ya Roho Mbaya na Matawi mengine yanayofanya vizuri," amesema Ahmed.
Akizungumza kuhusu mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravo FC kutoka Angola Ahmed amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kwakuwa uwepo wao ndio sababu ya ushindi.
"Ushindi wa mchezo dhidi ya Bravo hautotokana na Mo Dewji, Murtaza Mangungu au Fadlu Davids bali uwepo wetu sote Benjamin Mkapa siku hiyo utawaongeza morali wachezaji na tutawafanya vibaya vibaya Bravo," amesema Ahmed.