Simba Sports Club
News

Ahmed awapongeza VIP A Magomeni kwa kufungua Tawi

5 Sep 2025

Ahmed amesema mwanzoni walikuwa wanakutana uwanjani na kukaa pamoja lakini sasa watakuwa wanakutana tawini kwao na kupanga mambo yao kwa manufaa ya klabu.

“Niwapongeze kwa kufungua tawi hili, mwanzoni ilianza kama kikundi kukaa sehemu moja uwanjani baadae mkaungana na kuanza mchakato wa kufungua tawi. Ni jambo la kupongeza hongereni sana.

“Uwanjani tunakutana na kukaa kama familia, lakini inabidi kuwa na maisha mengine nje ya hapo, sasa mtakuwa mnakutana uwanjani na mkitoka wanakutana hapa kwenye tawi kuzungumza maisha mengine ya kuipeleka Simba mbele. Nawashauri wengine waige mfano huu, yapo makundi mengi ambayo wamekutana uwanjani na baadae wakaanzisha tawi," amesema Ahmed.

Advertisement

Ahmed ameendelea kwa kusema kuwa “Kuanzia sasa mnatakiwa kuishi kwa kufata miongozo ya Simba Sports Club, Viongozi na wanachama wa VIP A mnatakiwa kuipambania chapa ya Simba sio baada ya hapa tunakuja kuona mnaisema klabu halitakuwa jambo jema."

Kwa upande Mkurugenzi wa Wanachama, Mzee Hamis Kisiwa amewaomba Wanachama wote wa tawi hilo kujitokeza kwa wingi katika kushiriki shughuli za klabu ikiwemo Simba Day inayokuja.

“Hakikisheni kama tawi mnashiriki kila tukio la Simba. Simba haina baya, kila siku ina mazuri hivyo mjiandae kwa hilo, Jumatano tutakuwa na Simba Day mjaindae kikamilifu na mhakikishe wote mnakuja uwanjani katika siku hii muhimu," amesema Mzee Kisiw

Back to homepage
Share this story