Huu ni utaratibu wetu wa kuchangia damu kwa wenye uhitaji kila tunapoelekea kwenye Tamasha letu la Simba Day kila mwaka.
Hapa jijini Dar es Salaam zoezi hili la Uchangiaji Damu limefanyika katika sehemu mbili, Karume na Viwanja vya Mbagala, Zakhem ambapo Wanasimba wamejitokeza kwa wingi.
Akizungumza wakati zoezi hilo likiwa linaendelea, Ahmed amesema ni jambo la baraka mbele ya Mwenyezi Mungu kumsaidia mtu mwenye uhitaji hasa wa damu na ndio sababu kila mwaka tunapoelekea Simba Day lazima tutenge siku kwa ajili ya suala hili.
Ahmed ameongeza kuwa kuna Wanasimba wenzetu pamoja na Watanzania kwa ujumla wapo hospitalini na wanahitaji damu na sisi ndio ndugu zao wanao tutegemea kwa ajili ya kuwasaidia ndio maana kila mwaka tumakumbuka.
"Zoezi hili linafanyika nchi nzima, Wanasimba kutoka maeneo mbalimbali wameshiriki kikamilifu kwa ajili ya kuwasaidia ndugu zetu wagonjwa waliopo hospitalini."
"Sisi tunaichukulia kama sadaka kwa Mwenyezi Mungu pamoja na kurejesha kwa jamii. Kupitia sadaka hizi tunamuomba Mwenyezi Mungu atujalie tuwe na msimu mzuri," amesema Ahmed.