Simba Sports Club
News

Ahmed awaomba mashabiki kununua tiketi za Jumapili mapema

27 Sep 2023

Ahmed amesema Uwanja wa Azam Complex ni mdogo hivyo ili kuepusha usumbufu Wanasimba wanapaswa kuhakikisha wananunua tiketi mapema.

Ahmed ameongeza kuwa tumeweka viingilio rafiki ili kuwawezesha Wanasimba kujitokeza kwa wingi na kuujaza uwanja mapema kusubiri siku ya Jumapili.

"Viingilio tumeweka rafiki lakini pia tukubaliane uwanja wa Azam Complex ni mdogo unaingiza 7,000. Mashabiki wanaotaka kuwepo uwanjani wanunue tiketi mapema ili kuepuka usumbufu," amesema Ahmed.

Advertisement

Ahmed ametaja viingilio vya mchezo huo kuwa ni Mzunguko ni Tsh. 10,000, VIP Tsh. 30,000 na Platnum ni Tsh. 150,000 ambayo utapata zawadi, usafiri, chakula ukiwa uwanjani.

"Watu wanasema Chamazi ni mbali lakini kwa watu wa Platinum haitakuwa hivyo sababu watakuwa wana usafiri maalum utakaosindikizwa na escort," amesema Ahmed.

Back to homepage
Share this story