Ahmed ameyasema hayo katika soko la Temeke Stereo wakati wa zoezi la hamasa likiendelea baada ya kutoka Keko Maduka Mawili ilipozinduliwa.
Ahmed amesema kama Wanasimba tukiungana na kujitokeza kwa wingi hakuna namna Jwaneng Galaxy itatoka salama.
Advertisement
"Hii ni kwa Wanasimba wote, tunahitaji tujitokeza kwa wingi uwanjani ili kutimiza malengo ya kutinga robo fainali kwa mara ya tano mfululizo.
"Kila Mwanasimba anatamani kuiona Simba ikitinga robo fainali kwahiyo tunahitaji kushikamana na Jumamosi tujitokeze kwa wingi hakuna namna tutashindwa kutinga robo fainali," amesema Ahmed.