Simba Sports Club
News

Ahmed awaita Wanasimba wa Bombambili kwa Mkapa Jumatano

24 Nov 2024

Ahmed ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuzinduliwa na kwa Tawi hilo na ambapo amewaomba mashabiki na Wanachama kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi uwanjani siku ya Jumatano.

Ahmed ameongeza kuwa kwakuwa Tawi hilo bado ni changa hivyo Wanachama hao wanatakiwa kushiriki kikamilifu katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya klabu ikiwemo kujitokeza kwa wingi uwanjani mara kwa mara.

Advertisement

"Kwanza nichukue nafasi hii kuwakaribisha katika klabu yetu ya Simba na kwa sasa mnatambulika rasmi ila jambo la msingi ni kuhakikisha mnashiriki katika mambo ya maendeleo ya klabu."

"Na Jumatano mkija uwanjani hakikisheni mnakuja na bendera yenu kubwa ili Wanasimba wenzenu waweze kuwafahamu na mategemeo yangu ni kuwaona uwanjani kila timu itakapokuwa inacheza hasa nyumbani," amesema Ahmed.

Back to homepage
Share this story