Ahmed ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa wiki ya Simba ambayo safari hii imefanyika katika Uwanja wa Wambi, Mafinga mkoani Iringa huku akiwahakikisha hawatajutia kufanya uamuzi wa kwenda Benjamin Mkapa kwakuwa burudani itakuwa ya kutosha.
“Rasmi sasa tumeingia kwenye Wiki ya Simba na kilele chake ni Septemba 10, 2025, nataka kuona Wanasimba wote mnakuja Simba Day, asibaki mtu kila Mwanasimba aje twende tukafurahi pamoja.
"Tunawaalika Simba Day sio sababu ya kiingilio chako ila na nyie mje mfurahi, wale ambao wameshaonja raha hawawezi kuikosa, ukija utanishukuru hadi unakufa, kuna matukio mengi mazuri tumewaandalia," amesema Ahmed.
Kuhusu walionunua tiketi za fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mchezo ambao ulichezwa uwanja wa Amaan, Zanzibar Ahmed amesema “Wale walionunua tiketi mechi ya Berkane usinunue tena, utatumia ile tiketi yako lakini kama bado nenda ukanunue Simba Day ya mwaka huu sio ya kukosa."