Ahmed amesema moja ya nguvu inayotufanya kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika ni uwepo wa mashabiki hasa katika uwanja wa nyumbani.
Ahmed ameyasema hayo wakati akizungumza na Wanasimba wa Pugu Kinyamwezi ikiwa ni uzunduzi wa hamasa kuelekea mchezo huo muhimu ambao alama tatu ndio malengo yetu.
Advertisement
“Tuendelee kuhamasishana ili Wanasimba wengi waje uwanjani Jumapili hii kutokana na umuhimu wa mchezo huu. Mpinzani wetu ni mkubwa kwelikweli na silaha yetu ni mashabiki, na tunajua nguvu yenu mkiujaza Uwanja wa Mkapa."
“Kila Mwanasimba ni muhimu kununua tiketi na kuja uwanjani, kama kuna mtu hajawahi kuja uwanjani basi huu ndio uwe mtoko wao wa kwanza. Jumapili Novemba 23 tuje uwanjani lakini tuhakikishe tumevaa jezi za msimu huu," amesema Ahmed.