Simba Sports Club
News

Ahmed awaita Wanasimba kwa Mkapa Jumanne

16 Dec 2023

Ahmed ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa hamasa kuelekea mchezo zilizofanyika katika Viwanja vya Zakhem Mbagala.

Ahmed amesema kwa sasa kikosi kinaendelea kuimarika chini ya Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha na kila mmoja ameona jinsi wachezaji wanavyocheza kwa morali hivyo tunatakiwa kuhakikisha tunajitokeza kwa wingi uwanjani Jumanne.

Ahmed ameongeza kuwa pamoja na ubora walionao Wydad lakini watakapokuja kwa Mkapa na kukuta Uwanja umejaa na jinsi timu yetu ilivyo kwa sasa hawataweza kuepuka kipigo tena sio cha bao moja.

"Tumekuja hapa kwa lengo moja tu kuwaomba mje kwa wingi Jumanne katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuipa sapoti timu yetu. Tuna mchezo mgumu na unatuhitaji sote kwa kuwa kitu kimoja ili kufanikiwa kupata ushindi.

Advertisement

"Wydad ni timu nzuri lakini tumewahi kuifunga kwa Mkapa, sasa hivi tupo vizuri naamini kama tukiujaza uwanja hakuna namna tutashindwa kupata pointi zote tatu," amesema Ahmed.

Kwa upande wake Mwenyekiti wazamani wa Klabu, Mzee Hassan Dalali amewasisitiza mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani na kuendelea kumpa sapoti kubwa kocha Benchikha.

"Nimetazama mechi zote tatu za kocha mpya timu imeimarika nadhani sisi mashabiki tuendelee kumuunga mkono," amesema Benchikha.

Back to homepage
Share this story