Simba Sports Club
News

Ahmed awaita mashabiki KMC Complex kuikabili Mashujaa

30 Apr 2025

Ahmed amesema baada kufanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika sasa tunarejesha nguvu katika Ligi Kuu ya NBC tukianza na Mashujaa siku ya Ijumaa.

Ahmed amesema tayari kikosi kimerejea mazoezini kujiandaa na mchezo huo na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na morali zipo juu kuhakikisha tunazipata alama zote tatu.

"Baada ya Kombe la Shirikisho Afrika kufanya vizuri sasa tumerudi kwenye ligi ya nyumbani na Ijumaa tutakuwa na mchezo dhidi ya Mashujaa, nichukue nafasi hii kuwakaribisha mashabiki kujitokeza kwa wingi."

Advertisement

"Hii itakuwa mechi ya kwanza tangu timu ifanikiwe kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho hivyo itakuwa vizuri mashabiki mje kwa wingi kuwapongeza mashujaa wenu kwa kazi nzuri waliyoifanya," amesema Ahmed.

Katika kuthamini mchango wa wachezaji walioiwezesha timu kutinga fainali Ahmed amewaomba mashabiki wote kusimama wakati timu ikiwa inaingia uwanjani na kushangilia kama ishara ya kuwapongeza.

"Timu ikiwa inaingia uwanjani mashabiki wote tutasimama na kuwashangilia ili kuwashukuru kwa kutuwezesha kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika," amesema Ahmed.

Back to homepage
Share this story