Ahmed ameyasema hayo wakati akiongea na Wanasimba wa Arusha katika hamasa kuelekea mchezo huo ambao kwetu hatujitaji jingine zaidi ya ushindi.
“Sababu ya kwanza ya mechi ya kesho ni kulipa kisasi kwa namna walivyotupa sare kwenye mchezo wa Ligi Kuu. Tunataka watueleze ile sare walipataje, sababu ya pili tunataka kufuzu kutoka hatua ya 16 bora kwenda robo fainali. Lakini la tatu ni tunataka kushinda ubingwa wa Kombe hili.”
Advertisement
“Sababu hizi tatu zinatufanya tuingie katika mchezo wa kesho tukiwa serious kwelikweli tukitafuta matokeo. Na mimi niwambie ndugu zangu wa Arusha, hii ni kazi nyepesi mkiamua kusimama kidete, Mnachopaswa kufanya ni ninyi kwa uwingi wenu na kwa umoja wetu kwenda uwanjani," amesema Ahmed.