Ahmed amesema Tawi la Mo Simba Arena lina historia kubwa kwa klabu kwakuwa lipo nje Uwanja wetu na jambo jema ni kwamba limekidhi vigezo vinavyostahili.
“Binafsi ninayo furaha kuwepo hapa kwenye uzinduzi wa tawi hili. Niwapongeze Viongozi kwa kusimamia mchakato wote na hatimaye leo ndoto ya Bunju kuwa na tawi lake imekamilika na zaidi tawi hili limebeba jina la uwanja wetu wa Mo Simba Arena na nyie ndio walinzi rasmi wa uwanja wetu.”
“Watu wa Mo Simba Arena mna wajibu wa kulinda uwanja wetu, ni jukumu ambalo tumewapa leo. Ndugu zangu tupo kwenye Wiki ya Simba na ufunguzi wa matawi ni moja ya matukio kwenye Wiki ya Simba. Nipo hapa kuwakaribisha ndugu zangu wa Bunju kuja kwa wingi Simba Day. Viongozi fanyeni jitihada zote ili wote tukutane Uwanja wa Benjamin Mkapa,” amesema Ahmed.
Ahmed ameendelea kwa kusema kuwa “Wakristo wana Krismasi na Pasaka na Waislamu wana Eid lakini sisi Simba tuna Sikukuu yetu ya Simba Day. Kila mtu ahakikishe anashiriki Simba Day na kila mtu kushiriki kwahiyo tuhamasishane kila mmoja kuja uwanjani, wahi sasa kununua tiketi yako," amesema Ahmed.