Ahmed alitangaza ratiba ya uchangiaji damu kwa Wanasimba wote nchi nzima Novemba 20, ikiwa ni kwa ajili ya kuwasaidia ndugu zetu waliopo hospitalini pamoja na kumuomba baraka Mwenyezi Mungu ili kufanya vizuri katika mechi zetu.
Ahmed amesema mara zote Simba imekuwa na utaratibu wa kurejesha kwa jamii katika mambo mbalimbali na leo ilikuwa zoezi la kuchangia damu.
"Leo tumefanya zoezi la utoaji wa damu ambapo pamoja na kusaidia wenye uhitaji pia malengo yetu ni kumuomba Mungu atujalie katika michezo yetu hasa hii ya Kombe la Shirikisho Afrika," amesema Ahmed.
Akizungumza kuhusu hali ya kikosi, Ahmed amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na hakuna yeyote ambaye ni majeruhi.
"Kikosi chetu kipo kamili, wachezaji wanaendelea na mazoezi chini ya Kocha, Fadlu Davids na wasaidizi wake na jambo jema ni kwamba hakuna mchezaji yoyote majeruhi," amesema Ahmed.