Zoezi hilo limeanzia Magomeni, Buguruni Sheli, sokoni likapita Vingunguti mpaka Temeke Mikoroshini ambapo mashabiki na viongozi walikula biriani kabla ya kuelekea Temeke Stereo.
Katika sehemu zote tulizopita tumeuza tiketi za mchezo pamoja na jezi huku mwitikio wa mashabiki ukiwa wa kuridhisha.
Advertisement
Ahmed amesisitiza mashabiki kuendelea kununua tiketi mapema ili kuepusha usumbufu siku ya mchezo pia wapate nafasi ya kuingia mapema uwanjani kwa kuwa mchezo utakuwa saa 10 jioni.
"Mwitikio unavutia lakini bado naendelea kusisitiza watu wanunue tiketi mapema kupunguza usumbufu ambao unaweza kujitokeza," amesema Ahmed.