Rais Karia aliweka hadharani kuwa atavaa jezi ya timu inayocheza michuano ya kimataifa na atahudhuria uwanjani ikiwa ni sehemu ya kutoa mchango wake.
Baada ya kutoa kauli hiyo Menejimenti ya klabu ikaona ni jambo jema kumpatia jezi maalum ambayo ataivaa siku ya mchezo.
Advertisement
Simba inafarijika kuona kiongozi wa juu katika Mamlaka ya mpira nchini kujitoa kwa ajili ya kuhamasisha watu waziunge mkono timu zao za nyumbani huku akionyesha mfano.
Tumempa jezi namba 11 ikiwa ni kumbukumbu nzuri ya vipaumbele vyake 11 alivyovitoa wakati akigombea Urais wa TFF kwa mara ya kwanza mwaka 2017.