Morocco amesema itakuwa mechi ngumu lakini hatuna presha kwakuwa sio mara ya kwanza kukutana na nyakati hizi.
Morocco ameongeza kuwa wachezaji wapo kwenye hali nzuri na tayari kwa kuipigania timu ili kupata matokeo chanya ambayo yataivusha na kutinga hatua inayofuata.
"Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, na ninachotaka kuwaambia ni kwamba popote mtakapokuwa tumejiandaa kuwapa furaha," amesema kocha Morocco.
Advertisement
Kwa upande wake nahodha wa timu, Shomari Kapombe amesema wachezaji wote wapo tayari kufuata maelekezo watakayopewa na walimu ili kupatikana kwa ushindi.
"Kwa upande wetu wachezaji kwa ajili ya mchezo wa kesho, malengo yetu ni kufika hatua za mbele na ili kufanikisha lazima tushinde mechi hizi," amesema Kapombe.